Friday, 19 April 2019

PALAGYO APITA BILA KUPIGWA UBUNGE JIMBO ARUMERU MASHARIKIMbunge mteule Wa jimbo la Arumeru mashariki Dr. John Pallagyo akiongea na waandishi Wa habari katika jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mara baada ya kuteuliwa kuwa mbunge.

Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha

Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi John   Pallagyo amepita bila kupigwa katika uchaguzi Mdogo Wa jimbo la Arumeru mashariki Mara baada ya wagombea wenzake   10 kukosa sifa .

Akizungumza akitangaza matokeo hayo msimamizi Wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi Wa halmashauri ya Meru  Emmanuel mkongo alisema kuwa jumla ya wagombea 11 walichukuwa fomu ya kugombea ubunge Wa  jumbo hilo na wagombea Tisa wamerejesha fomu hizo huku wagombea watatu wakiwa hawajarejesha kabisa

Alisema kuwa  wagombea hao Tisa wameshindwa kupitishwa katika kinyanganyiro hicho kutokana nakukosa sifa  na kutotimiza mashariti ya uchaguzi.

Baadhi ya wagombea hao ambao wameshidwa kukithi vigezo ni pamoja na wagombea watatu ambao hawakuteuliwa kwasababu hawajarudisha fomu ,huku wengine wakiwa saba wakiwa wamerejesha lakini hawajakizi vigezo vikiwemo ,kutolipa thamana ya kugombea   ubunge  ambayo inagharimu shilingi elfu 50 ,kukosa wathamini pamoja na kuleta hati ya kula kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Alisema katika fomu hizo fomu moja tu ndio ambayo ilikuwa haina mapungufu ya kisheria hivyo alitumia  nafasi hiyo kumtangaza John Pallagyo  kupita bila kupigwa na kuteuliwa kuwa mbunge Wa jimbo la Arumeru mashariki .
 
Akizungumza   leo  ofisi za halmashauri ya wilaya ya Meru, mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge mteule kupitia chama cha mapinduzi, John Pallagyo amesema kuwa, ameshukuru Sana Kwa hatua hiyo kwani imekuja kama muujiza kwake pia ameshukuru viongozi wa ngazi zote ambao walionyesha imani kwake na kuhakikisha jina linarudi kwenye kinyanganyiro hicho. 

"Kitu cha kwanza nitakachofanya nipamoja na kuhakikisha  Barabara zinatengenezwa kwani Jimbo hili halina barabara kabisa, sambamba na maji,  pamoja na umeme kwani wananchi wa Jimbo hili wameteseka Kwa muda mrefu sasa. "alisema Pallagyo. 

Aidha pia alisema kuwa kwa vile Amelita kitu cha kwanza atakachomuomba rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania ni kutimiza ahadi yake ambayo aliwahaidi wananchi Wa Meru kipindi alipopita kuomba kura mwaka 2015  ya kuwajengea wananchi Wa Meru barabara kilometa tano kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wa mgombea mwingine kupitia chama cha AAFP, Mgina Ibrahimu ambaye ni Mwenyekiti wa vyama vya siasa wilaya ya Meru, amesema kuwa, kwa upande wake yeye ameshindwa kurejesha fomu kutokana na kutoridhika Kwa mwenendo mzima wa uchaguzi katika Jimbo hilo. 

Amesema kuwa, akiwa Kama Mwenyekiti wa baadhi ya vyama vya siasa, hawajatendewa sivyo kutokana na baadhi ya vyama kupewa fomu na vingine kutopewa fomu kikiwepo chama cha UMP, na UDP wakati vilikuwa na haki. 

Naye Mgombea mwingine wa chama cha SAU, Shafii Mohamed amesema kuwa, anakishukuru chama chake Kwa kumpitisha yeye kuipeperusha bendera ya chama hicho. 


Amesema kuwa, ana imani na tume ya uchaguzi kuwa haki imetendeka  na wameweza kumtangaza mgombea aliyepita Kwa kufuata kanuni na sheria za uchaguzi. 


No comments:

Post a comment