Tuesday, 30 April 2019

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA WAFANYAKAZI VIJANA KUSHIRIKI KATIKA UCHUMI WA VIWANDA


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka Wafanyakazi Vijana kushiriki katika uchumi wa Viwanda kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali hasa KILIMO na UFUGAJI.

Mavunde ameyasema hayo jana kwenye Chuo cha Wafanyakazi Mbeya,wakati akifungua semina ya wafanyakazi Vijana waliomo kwenye sekta ya Umma ambao pia vyama vyao ni wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)

“Pamoja na kuwa mna ajira tayari kwenye sekta ya umma,lakini bado hamzuiwi kujihusisha kwenye shughuli za uzalishaji mali hasa kwenye sekta za kilimo na ufugaji ambazo zina mchango mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa Viwanda hapa nchini”

Akimkaribisha Naibu Waziri Mavunde,Makamu wa Rais wa TUCTA Ndg. Qambos Sule amesema Shirikisho limejipanga kushiriki katika uchumi wa Viwanda kwa vitendo na hivi sasa wamepata washirika kutoka China na Uturuki kwa lengo la kuwajengea uwezo wafanyakazi wake na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uchumi wa viwanda.

No comments:

Post a comment