Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewataka askari wa misitu waliohitimu mafunzo ya kijeshi kuhakikisha wanarejesha uoto wa asili katika maeneo yote ya misitu ambayo yameharibiwa.

Mhe. Kanyasu ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kijeshi kwa askari 140 wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kambi ya mafunzo ya kijeshi Mlele mkoani Katavi. “Leo mmehitimu na tumewaapisha, mmekuwa askari kweli wa TFS lakini tambueni kuwa kazi za kiuchumi zinapelekea uharibifu mkubwa sana wa mazingira, na hatuwezi kusema zisiendelee! Zinatakiwa kuendelea katika namna ambayo haitaifanya nchi yetu kuwa jangwa.

Amesema ni matarajio ya Serikali baada ya askari hao kuhitimu pamoja na kazi yao ya msingi ya ulinzi watafanya kazi ya kuhakikisha wanarejesha uoto wa asili uliopotea.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: