Naibu Spika wa Bunge, Dr Tlia Ackson amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuripoti kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na kauli yake kuwa "Bunge ni dhaifu". 

Lema ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, 2019  Bungeni wakati akichangia hoja ya kamati hiyo na kudai Halima Mdee hajatendewa haki kutokana na kamati hiyo kupendekeza Bunge kumsimamisha kuhudhuria vikao viwili vya Bunge kutokana na kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa Bunge ni dhaifu

"Alichokisema Mdee naungana naye na ni kweli kuwa Bunge ni dhaifu," amesema Lema. 


Baada ya kauli hiyo, Naibu Spika  Dk Tulia ameagiza Lema akahojiwe  na kamati hiyo ya Maadili  kwa kuliita Bunge ni Dhaifu.

Kutokana na Maamuzi hayo ya Naibu Spika, Wabunge wote wa CHADEMA na Baadhi ya Wabunge wa CUF wametoka nje ya ukumbi wa Bunge
Share To:

msumbanews

Post A Comment: