Wednesday, 10 April 2019

DKT. MPANGO KATIKA MIKUTANO YA BENKI YA DUNIA NA IMF-WASHINGTON DC.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (katikati) akiongoza kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya  Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Khamis Mussa Omar na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.

Dkt. Mpango (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi wakati wa kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mjini Washington DC.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi, akizungumza jambo wakati wa kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mjini Washington DC.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, akiwa katika kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mjini Washington DC.

No comments:

Post a comment