Cameroon yatwaa ubingwa wa kombe la Total AFCONU17 kwa kuifunga Guinea penati 5-3 baada ya timu hizo kushindwa kufungana katika dakika 90.

Itakumbukwa kuwa Serengeti Boys ilitolewa kwenye michuano hii mapema kwenye hatua za awali baada ya kufungwa mechi zote tatu za kundi A na kumaliza ikiwa nafasi ya nne bila kuambulia pointi hata moja.

Michuano hiyo iliyoshirikisha timu nane leo imefika tamati uwanja wa Taifa na kushuhudia bingwa akiwa ni Cameroon aliyeibuka kidedea baada ya kushinda mbele ya Guinea.

Mchezo huo uliochezwa leo dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kumaliza bila kufungana na ndipo bingwa akapatikana kwa mikwaju ya penalti ambapo Camareoon walishinda penalti 5-3.

Timu nne ambazo zilitinga hatua ya nusu fainali ambazo ni Nigeria, Angola, Guinea na Cameroon zimevimba akaunti zao kwa kuingiza dola 75,000 (Tsh. 173,472,656), bingwa ambaye ni Cameroon amesepa na dola 150,000 (Tsh.346,954,144) na mshindi wa pili Angola ambaye alimshinda Nigeria jana kwa mabao 2-1 anavimba na dola 100,000 ( Tsh.231,302,752).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: