SERIKALI YA CHINA WAAHIDI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI - MSUMBA NEWS BLOG

Tuesday, 23 April 2019

SERIKALI YA CHINA WAAHIDI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI


Na WAJMW-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe kutoka jimbo la Shadong la nchini China katika ofisi za Wizara zilizoko Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika mbele ya wajumbe wa kikao cha Menejimenti yalilenga kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na China, Dkt. Chaula amesema wamekubaliana kushirikiana katika kubadilishana uzoefu na kuzalisha wataalamu wa afya waliobobea katika sekta mbalimbali.

“Kimsingi tumekubaliana na wajumbe hawa toka jimbo la Shadong lililopo China kuendelea kushirikiana katika kuboresha sekta ya afya nchini na kwa kuanza tumesaini makubaliano ya kusomesha Watanzania madaktari bingwa kwenda kusoma kozi mbalimbali kwa muda mrefu na muda mfupi”. Amesema Dkt. Chaula.

Dkt. Chaula amesema lengo la makubaliano hayo ni kuhakikisha Tanzania inapata wataalamu wa afya wabobezi watakaosaidia katika kuboresha huduma za kibingwa nchini mara baada ya kusoma kozi mbalimbali za kada ya afya chini China.

Nae Dkt. Ligile Vumilia ambaye ni mratibu wa ushirikiano wa Tanzania na China kwenye eneo la Sekta afya ambayo chini ya idara ya tiba amesema jimbo la Shadong limekua likileta wataalamu chini katika sekta ya afya kuanzia miaka ya 1960 na wamekua wakihudumu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za mikoa ya Tabora, Dodoma na Mara.

Dkt. Vumilia amesema timu iliyokuja ni ya viongozi ambayo itasaidia kuendeleza uhusiano kwa kuleta vifaa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya JKCI, kuleta madaktari wanaotoka China kwa ajili ya kutoa huduma nchini na pia kutoa fursa kwa madaktari bingwa 50 nchini kwenda kusoma China na kuongeza ujuzi zaidi.

Aidha, Dkt. Vumulia amesema ujumbe huo utasaidia kuleta vifaa tiba ambavyo vitasaidia katika kutibu magonjwa ya moyo nchini, pia ugeni huo utasaidia kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano katika Mji wa Serikali eneo la Wizara ya Afya  utakaoitwa Shadong ambao utatumika katika masuala mbalimbali ya elimu ya afya (tiba mtandao) ambapo Katibu Mkuu na uongozi watakua na uwezo wa kuwasiliana na madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Rufaa za mikoa na Kanda pasipo wao kufunga safari.

MWISHO
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done