Thursday, 21 March 2019

SERIKALI IMEAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA JENGO LA UTAWALA KATIKA SHULE YA ARUSHA SEKONDARI NA KUONGEZA MCHEPUO WA PCM.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo katika maafali ya 21 ya kidato cha sita katika shule ya Arusha.

Aidha  Gambo ameeleza kuwa mbali na changamoto nyingi za shule hiyo hususani uwepo wa mabweni ya kiume ameahidi kushilikiana na viongozi wenzake kuweza kuondoa changamoto hiyo ya mabweni pamoja na nyumba za walimu zinatatuliwa.

Pia ametoa ahadi ya kumsomesha mwanafunzi atake fanya vizuri katika shule hiyo  kwa kupata daraja la kwanza kwa alama ya pointi 3 hadi 5 atasoma digrii yake ya kwanza nchini china na kuwataka wanafunzi wote nchini wa kidato cha sita kuachana na makundi mabaya yanaweza kupelekea kuaribu taaluma zao walizo zipata.Awali akianisha changamoto za wanafunzi wa shule hiyo mmoja wa wanafunzi wa kidato cha sita Salma Maulid ameeleza kuwa ukosefu wa bweni ya wanafunzi wakiume kitu kinachopelekea wanafunzi wengi wa kiume kutofika kwa wakati darasani na kukuta vipindi vikiendelea.


Pia upungufu wa choo na udogo wa mactaba ni changamoto na huku maabara za sayansi ni chache na kupelekea kutokua fursa kwa masomo ya sayansi nakuunga juhudi za serikali kwa kupata wataalamu wa sayansi kwa maendeleo ya nchi yetu kufikia Tanzania ya viwanda ambapo wameiomba serikali iweze kuongeza habara hizo za sayansi.


Nae kwa upande wake mkuu wa shule ya Arusha sekondari Ndg Christofa Mallamsha ameeleza kuwa Mpaka sasa mkakati wa shule ni kuondoa ufaulu wa daraja la nne na kuongeza elimu ya sayansk ili kuendana na changamoto ya taifa kwa kuhitaji wataalamu wa sayansi.


Aidha pia amemshuku mkuu wa mkoa Arusha kwa kuanzisha mitihani ya kila mwezi kwa vidato vyote kitu kinacho changia ufaulu kwa asilimia zaidi ya 95 pia ameeleza changoto za shule yake ikiwemo changamoto ya walimu wa sayansi,ukosefu wa nyumba za walimu na kubwa zaidi ni jengo la utawala.


Mitahani hiyo ya kidato cha sita inatarajiwa kuanza 6 may 2019 huku shule ya Arusha Sekondari ikiwa na wanafunzi 157 wanao tarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu elimu hiyo.No comments:

Post a comment