Tuesday, 26 March 2019

MRADI MKUBWA WA MAJI KUMALIZA KERO YA MAJI JIJINI ARUSHA

 Mkurugenzi mtendaji AUWASA Mhandisi Ruth Koya (mwenye shati light blue) akiwa sambamba na Kamati ya Kudumu ya Bunge walipotembelea mradi huo uliopo Murieti/Terati Jijini Arusha.
 Meneja wa Mradi wa Kutibu majitaka uliopo Muriet /Terati ndugu Niny Yunfeng kutoka kampuni ya China Civil Enginearing Construction akizungumza na waandishi wa habari katika eneo ambalo mradi upo na kuelezea naendeleo ya mradi kwa ujumla.
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari kubusiana na mradi mkubwa wa. Maji unaotekelezwa Jijini Arusha sambamba na kuishukuru kamati ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji
Mshauri na muelekezi wa mradi wa Maji moto uliopo hai mkoani Kilimajaro,jiologisti Profesa Mkulo akitoa ufafanuzi kwa Kamatibya bunge namna mradi huo unavyotekelezwa. 
 Injinia Jailos chilewa ambae ni Mshauri muelekezi wa mradi  ujenzi wa tank la maji Ngaramtoni mkoani Arusha akiwaonyesha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji walipotembelea kukagua mradi huo umefikia kiwago gani.
 Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akiwa pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakionyeshwa mchoro wa ujenzi wa Matenki yakubw ya maji yanayojengwa Ngaramtoni.
 Baadhi ya wakandarasi wa Miradi hiyo mkubwa wa majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha na baadhibya maeneo ya wilaya ya Arumeru unaotekelezwa na AUWSA, Seed farm, SewerNetwork outside CBD, WSP.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge akisoma ramani kwa makini ya mradi wa kutibu majitaka uliopo Murieti/Terati.

Mkurugenzi mtendaji wa AUWSA Mhandisi Ruth Koya akitoa ufafanuzi kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji walipotembelea moja ya Kisima cha majimoto ambapo mradi mkubwa wa maji unatekelezwa kilichopo Rundugai wilaya ya Hai


Na. Vero Ignatus, Arusha

Serikali imefanikiwa kupata mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Afrika (AfDB) kwa jumla ya shilingi Bilioni 514 (233.9mil.USD) kwaajili ya kuboresha huduma ya majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru

Mhandisi Ruth Koya ni  Mkurugenzi mtendaji AUWSA anasema Mradi huo mkubwa wa maji utaondoa kero ya upungufu wa maji kwani uboreshaji wa huduma utaongezeka kutoka wastani wa lita 40,000,000 hadi lita
200,000,000,kuongezeka kwa wakazi wanaopata maji toka wastani wawatu 325,000 hadi kufikia 600,000 wakiwemo wastani wa watu 250,000 wanaoingia na kutoka Jijini kila siku

''Hii Itapunguza maji yanayopotea kutoka wastani wa 40%hadi25% kuongeza mtandao wa bomba za majisafi kutoka 44%hadi 100%

Mhandisi Koya anasema lengo la mradi ni uboreshaji wa huduma ya usafi wa mazingira na miundombinu yake kuongeza mtandao wa ukusanyaji wa maji taka kutoka 7.66% hadi 30%,kujenga mabwawa ya majitaka, kupunguza kero ya uzibaji wa mabomba, kutoa elimu ya usafi wa mazingira. 

Utafiti wa vyanzo vya maji uliofanywa na kampuni ya Engis kutoka Ufaransa umebaini kwamba chanzo kikuu cha maji kwasasa katika jiji la Arusha ni visima virefu, ambapo umebainisha maeneo ya uchimbaji eneo la Magereza-seed-Farm, Tengeru-Makumira, Usariver, Valeska - Mbuguni  na Majimoto iliyopo Hai mkoani Kilimanjaro. 

Mkuu wa wilaya ya Arusha  Gabriel Daqqaro amesema wanamshukuru mhe. Magufuli 2018 alivyokuja kuzindua mradi huo wa maji, amesema yapo maeneo mengi ambayo yana shida ya maji ila serikali yake imeona Arusha ndiyo jiji linalohitaji mradi mkubwa    kufuatia na ule wa Tabora

Amesema kupitia mradi huu wananchi wa Arusha watakwenda kupata maji kwa 100% tofauti na 44%ya sasa kwamba wanapata milioni 60 wa siku  kwa kipindi cha kiangazi lakini lita zinazo hitajika kwa siku ni lita milioni 94 mradi huu unatuhakikishia kwamba upatikanaji wa maji kwa jumla ya lita milioni 200 kwa siku hivyo tutakuwana akiba ya maji ya kutosha kwa kipindi kirefu.

Tunaihakikishia serikali sisi kama wilaya tutaendekea kuisimamia hii miradi tutailinda, na kuitunza na kuhakikisha miradi hii haihujumiwi na mtu yeyoye na kwenye  vyanzo vyetu vya maji vingine vipo nje ya wilaya vingine ndani tutahakikisha tunashirikiana na serikali za kule kuhakikisha vipo salama.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo, mifugo na maji Mahamood Mgimwa Mb (Mufindi Kaskazini) amesema wanaiomba serikali kutupia macho eneo  la TRA kutokuachia mabaomba ambayo yapo kwao kwa takribani miezi 2 yanayochelewesha watu kupatiwa maji

'' Mradi mkubwa wa maji ameuzindua Rais  yeye mwenyewe unacheleweshwa bila kuwa na sababu za msingi huo ucheleweahaji usingelikuwepo leo watu wangelikuwa wanapatiwa maji baadhi ya maeneo''alisema

Ameyataka makampuni yaliyopewa tenda kwenye hiyo miradi yafanye  kazi kwa ufanisi na kwa haraka amewataka kutokuwaingiza kwenye matatizo kwani mwaka 2021 pesa zinatakiwa zianzwe kulipwa zilipokopwa

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema utekelezaji wa mradi huo wa maji unatekelezwa na wakandarasi 10 na wote wanahitaji msamaha wa kodi ambapo maombi yote yaliwasilishwa serikalini na yamefanyiwa kazi na hadi sasa misamaha 4 imeshapatikana kulingana na jinsi wanavyowasilisha na mingine inatendewa kazi na wakati wowote misamaha hiyo itapatikana

'' Vitu amabavyo vinachanganya katika upatikanaji wa misamaha ya kodi ni ukamilifu wa maombi yeyewe ambayo hayajakidhi vigezo vyenyewe kwasababu maombi mengine tamekuwa yakija yanarudi kwasababu hajajakidhi vigezo vyote, lakini mwombaji yeye kwasababu ameshawasilisha anaona kwamba amechelewa haesabu ule muda kwamba alirudishiwa ili afanya masahihisho.

Amesema serikali imeshaweka utaratibu mzuri wa kushughulikia misamaha kwa miradi yote mikubwa ambayo imeshaainishwa kwamba inahitaji kupata msamaha na kama Wizara wanaendekea kufuatilia kwa karibu maombi yanayowasilishwa

Amesema ameneo yote ambayo maji yatapitia wataachiwa maji kama sera ya maji inavyosema lakini pia bomba linapopita kama sera ya wizara isemavyo kilometa 12 kushoto na kulia watu wale lazima wapate maji

Mwenyekiti wa Bodi ya majisafi na Usafi wa mazingira Jijini Arusha Mhandisi Dkt. Richard Masika amesema kuwa mradi huo utaongeza uzalishaji wa maji kutoka milioni 93 hadi lita milioni 200 itaondoa kabisa tatizo la maji katika jiji la Arusha pamoja na baadhi ya maeneo ya Arumeru

Amewaomba wananchi  waendelee kupata ushirikiano katika maeneo ambayo kazi zinaendelea wawe na uvumilivu kwasababu kila kazi inataratibu zake

Nae Meya wa Jiji la. ARUSHA Kalisti Lazaro ameishukuru Serikali kwa kuona Jiji la Arusha wanastahili kupata mradi huo mkubwa wa maji amesema kwao  ni heshima kubwa kwao

Amesema kwajinsi hali inavyoelekea historia ya tatizo la  maji katika jiji la Arusha itakuwa imesahaulika

No comments:

Post a comment