Monday, 1 April 2019

MAJALIWA ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA BAJETI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Machi 31, 2019 kushiriki katika Kikao cha Mashauriano kati ya Kamati ya Uongozi  na Kamati ya Bajeti kuhusu mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati  za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti  za Wizara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma.  Wa pili kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango  na katikati ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, William Tate Ole Nasha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  Machi 31, 2019 alishiriki  katika Kikao cha Mashauriano kati ya Kamati ya Uongozi  na Kamati ya Bajeti kuhusu mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati  za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti  za Wizara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza katika Kikao hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a comment