Wakazi wa Kisiwa Kodogo Cha Chole Wilaya Ya Mafia  Mkoani Pwani Wameiomba Serikali Kufanya Juhudi Za Makusudi Kuiokea Shule Ya Msingi Chole  Baada Kuondokewa  Na Walimu 4 Na Kubakia Na Walimu Watatu Ambao Hawatoshelezi Mahitaji Halisi Ya Shule Hiyo  

Wakingumza Na  Global Tv Kijiji Hapo Wamesema Watoto Wao Ambao Wanatarajia Kufanya  Mitihani Yao Ya Mwisho , Asa  Kwa Wanafunzi  Wa Darasa La Saba Wapo Katika Hatari Kubwa Ya Kuferi  Mitihani Hiyo  Kwa Kuwa Hawapati Vipindi Vya Kutosha Kutokana Na Uhaba huo Wa Walimu.

Shule Hiyo Yenye Mikondo Ya Darasa La Kwanza Mpaka la Saba Imebakiwa Na Waalimu Watatu Kwa Sasa Wanaofundi Baada ya Wangine Wanne Kuomba Uhamisho Kwa Mkupuo  Kwa Mujibu Wa Sheria.

Diwani wa Kata Ya Jibondo Bwana Hassani Mohamed Anasema Pamoja Na Mazingira Mazuri Waliyoyaweka Katika Shule Hiyo Yaupatikanaji Wa Maji Na Nyumba Za Walimu Lakini bado Walimu Hao Wameomba Uhamisho Na Kuondoka Zao.

‘’Nilichogundua Tatizo Lipo Kwa Halmashauli Yetu Wamekuwa Wakiwaacha Walimu Wanakaa sehemu Moja Kwa kipindi kirefu uku Visiwani Hali Inayopelekea Waalimu Kuomba Uhamisho Kwa Sababu Wanakosea Mambo Mengi Ya Kujiliwaza Asa Ukizingitia Uku Visiwani Hakuna Vitu Vingi Vya Kujiliwaza’’ Alisema Mhe Diwani Uyo.

Nae Mratibu Elimu Kata Ya Jibondo Khamis Pazi Anasema Shule Hiyo Yenye Mahitaji Ya Walimu 8 Kwa Sasa  Inapitia Wakati Mgumu Kwa Kuwa  Kitakwimu Shule Hiyo Ina Walimu 4 Kwa Hivi Sasa Lakini Kati Ya Hao  Wanne  Mmoja  Ni Mwalimu Mkuu  Ambae Kwa sasa  Yupo Likizo Ya Uzazi.

Akielezea Zaidi Mratibu Elimu kata Anasema Waalimu Waliopo Sasa Mmoja Ni Mwalimu Wa Darasa La Awali Na Walimu Wawili Waliobakia  Wanafundisha Mikondo Yote Inayobakia Hali Ambayo Inasababisha Kukosa ufanisi Katika Ufanyaji Kazi Wa Kila Siku Hali Inayopelekea Waalimu Waliopo Kubeba Mzigo Mkubwa  Wa Vipindi Kila Siku.

Nae Mbunge Wa Jimbo Ilo La Mafia Mbaraka Dau  Amesema Kwa Kushirikiana Na Mkurungenzi Wa Hamashauli Hiyo  Wanatafuta Ufumbuzi  Wa Jambo Ilo Kwa Kujua Idadi Ya Walimu Wanaopatikana  Katika Kisiwa Cha Icho Cha  Mafia.

 Na  Kama kuna Shule Ina Waalimu Wengi Wafanye Utaratibu  Wa Kuhamishia Shule Ya Msingi Chole Ili Kuziba  Nafasi  Hizo, Lakini Pia  Amewasiliana Na Waziri Seleman Jafo  Wa Tamisemi Ambae Ndie Mwenye Dhamana Awapatie  Waalimu Ili Kumaliza Tatizo Ilo.

Nae Mkurungenzi Wa Halmashauli Hiyo Mafia Bwana Erick Mapunda Amesema Sababu kubwa Inayosabisha Watumishi  Mbalimbali Wanaopangiwa Wilaya Ya Mafia kuomba Kuhama Ni Kutokana Na ukosefu Wa Usafafiri Wa uhakika.

Wilaya Ya Mafia Inakabiliwa Na changamoto Ya Usafiri Kwa Kukosa Meli Inayofanya Kazi kila siku Ambapo Wananchi wa wilaya Hiyo wamekuwa Wakitumia Boti Za Uvuvi ambazo Si Salama Kwa Wasafiri Au Kutumia Ndege Ambazo Gharama Zake Ni Kubwa Ambazo Wananchi Wamekuwa Wakishindwa Kuzimudu 
Wilaya Ya Mafia Inakabiliwa Na Kukutwa Na Janga La Ukosefu Wa Watumishi Kwa Kuwa  Kwa Mujibu Wa Mgurungenzi wa Halmashauli Erick Mapunda Anasema Maombi Ya Watumishi Wanaomba Kuhama Ni Mengi Kuliko Wanaingia Wilayani Mafia, Ambapo Wilaya Hiyo Mpaka Sasa Ina Mapungufu Ya Ya Watumishi Katika Idala Ya Elimu Ya Waalimu 119, Na waliopo Ni 257, Na Mahitaji Wilaya hiyo Hinahitaji Jumala Ya Waalimu 373 Kutosheleza Shule 6  Za Sekondali Moja Ya Kidato Cha Tano Na Shule Za Msingi  15
Share To:

msumbanews

Post A Comment: