Wednesday, 8 August 2018

PICHA: Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo azindua Operesheni Jokate yenye lengo la kuwaondoa wavamizi Wote Misitu ya Ruvu

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amezindua "Operesheni Jokate"yenye lengo la kuwaondoa wavamizi wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na Kazimzumbwi wilayani humo. 

Jokate alizindua oparesheni hiyo   jana Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa Ruvu Kusini ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu ( TFS) kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi waliopo humo.

Alisema lengo lake ni kuwasaka na kuwaondoa wavamizi ambao hawataki kufuata sheria na utaratibu wa hifadhi ya misitu katika msitu wa Ruvu Kusini uliopo wilayani humo.

Jokate alisema operesheni hiyo ni ya siku sita na imeanza  Agosti 7 ambapo katika siku ya kwanza ng'ombe zaidi ya 150 walikamatwa ndani ya msitu huo na zoezi la kuwakamata wamiliki wake linaendelea.No comments:

Post a comment