Thursday, 19 July 2018

Ndalichako aitaka TCU kuongeza ubora wa vyuo vikuu


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ameiagiza Tume ya vyuo vikuu nchini TCU kuongeza kasi ya kuhakiki ubora wa vyuo vya elimu ya juu na vitakavyobainika kukosa vigezo hata kiwe cha serikali kifungiwe kwani suala la ubora wa elimu  ni jambo la lazima kwani  hakuna haja ya kuwa na msururu  wa vyuo visivyokuwa na tija.

Prof Ndalichako ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonyesho ya vyuo vikuu ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.

Wakati akizindua maonyesho hayo Prof Ndalichako amevitaka Vyuo vikuu kutafuta suluhu changamoto zinazoikumba jamii  na  kuonyesha fursa  mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo,viwanda ambapo baadhia ya vyuo vimemweza kuhusu tafiti walizofanya katika maeneo hayo.

Katika maonyesho hayo baadhi wanafunzi wamejitokeza kupata taarifa za namna ya kujiunga na vyuo vya ndani na nje ya nchi na kupatiwa maelezo ya kina.

No comments:

Post a comment