Watanzania wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini kwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kulipa kodi ili kuiwekeza Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mahojiano ya kipindi maalum na Redio Boma FM Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro na kuwataka wananchi kuiachia Serikali yao iwatendee haki ya kikatiba katika kuwaletea maendeleo yaliyokusudiwa.

Dkt. Abbasi alisema Watanzania kwa sasa wamepata Serikali makini na sikivu inayowajibika kwa wananchi wake kwa kuwa imeweza kuelewa matatizo na kero mbalimbali za muda mrefu zilizokuwa zikiwakabili katika jitihada zao za kujieletea maendeleo.

Alisema tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kumekuwa na shabaha mbalimbali zilizowekwa ikiwemo malengo ya kuwa na nchi ya uchumi wa viwanda ambayo hata hivyo ilishindwa kufikiwa lakini kwa sasa imefanikiwa katika Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliongeza kuwa yapo maendeleo makubwa yanayoendelea kufanyika katika sekta zote za maendeleo nchini hususani kupitia miradi mikubwa inayogusa maisha ya kila siku ya wananchi ikiwemo nishati, maji, elimu, afya na kadhalika ambapo tayari mageuzi yake yameanza kuleta matokeo chanya kwa Watanzania walio wengi.

“Kwa kipindi kirefu tumekuwa na kilio cha umeme wa uhakika hususani kwa wananchi wa vijijini, lakini tunapozungumza kwa sasa Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya umeme ikiwemo Kinyerezi I na kuongeza upanuzi wa megawati kutoka Megawati 150 hadi 185, ni umeme mkubwa unaoweza kulisha mikoa mingi zaidi” alisema Dkt. Abbasi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: