Zaidi ya Kampuni 70 za ukandarasi zimejitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali za Dar es salaam Bure kama sehemu ya kuunga mkono jitiada za Mkuu wa mkoa huo  Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda kufanya ziara usiku na mchana na kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo.

Makonda amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka  kwa Meneja wa TARURA Wilaya kwaajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo.

Aidha  Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo Bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya pesa za serikali.

Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: