Monday, 21 May 2018

TIBWA SUGAR RASMI YAISHUSHA DARAJA NJOMBE MJI IKIWA KWAO


Kikosi cha Mtibwa Sugar kimepeleka maumivu mjini Njombe kwa kuifunga Njombe Mji FC bao 1-0 na kuondoa rasmi ndoto za kuendelea kusalia kunako Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Bao pekee la Mtibwa katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe limepachikwa kimiani na Hassan Dilunga mnamo dakika ya 81 kipindi cha pili.

Matokeo hayo yamepokelewa kwa uchungu mkubwa kwa Wanajombe kufuatia timu yao kuondoshwa kwenye ligi na sasa itashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Ushindi wa Mtibwa umezidi kuiweka kwenye 10 bora ambapo mpaka sasa imefikisha pointi 40 kwenye nafasi ya 6 ya msimamo wa Ligi.

No comments:

Post a comment