Wednesday, 16 May 2018

TFF yalikubali Ombi la Simba

Kufuatia maombi ya Simba kuomba viingilio vya mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Mei 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, TFF imeridhia ombi hilo.

Kupitia Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema kuwa wameamua kupunguza kiingilio hicho kwa sehemu ya mzunguko ambayo ilikuwa imepangwa kuwa 3000 na badala yake itakuwa 2000.

Kidao amefunguka wameamua kufanya hivyo ili kuwapa nafasi mashabiki kujitokeza Uwanjani kwa wingi, ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Magufuli atahusika katika kuwakabidhi Simba kombe la ligi walilotwaa msimu huu sambamba na kupokea pia taji la CECAFA waliloshinda vijana wa Serengeti Boys huko Burundi.

Baada ya kupunguzwa kwa viingilio hivyo, viingilio vya sehemu zingine zilizosalia vitabakia kama vilivyopangwa.

No comments:

Post a comment