Friday, 11 May 2018

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO IJUMAA YA MEI 11 2018

Mshambulijai wa Liverpool Mohamed Salah amesema kuwa hataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Raia huyo wa Misri mwenye umri wa miaka 25 amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Real Madrid (Mirror)
Kiungo wa kati wa Ivory Coast Yaya Toure, 34, atakataa maombi kutoka China na mashariki ya kati kuendelea kucheza kwa kiasi kidogo cha fedha katika ligi ya Uingereza wakati atakapoondoka Manchester City mwisho wa msimu huu. (Mail)
Manchester City inaongoza katika kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Napoli Jorginho. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Itali pia anasakwa na timu sita bora za ligi ya Uingereza (Times)
Atletico Madrid inataka kumsaini mshambuliaji Sergio Aguero kutoka Manchester City. Raia huyo mwenye umri wa miaka29- aliondoka Madrid 2011. (Mail)
Everton inaandaa dau la £25m kumnunua beki wa Newcastle na nahodha wake Jamaal Lascelles, 24. (Mirror)
Mkufunzi wa timu ya Uingereza Gareth Southgate anapima kumshirikisha beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, 19, na winga wa Fulham Ryan Sessegnon, 17, katika kikosi chake cha wachezaji 35 cha kombe la dunia (Telegraph)
Juventus inajiandaa kuwasilisha ombi la £15m kwa klabu ya Chelsea ili kumnunua mshambuiliaji Alvaro Morata, 25, kwa mkopo. (Express)

Kutoka BBC

No comments:

Post a comment