Sunday, 20 May 2018

Salome ya Diamond ‘yamuweka kifungoni’ Hamisa Mobetto

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka ni kwanini siku hizi hatokei tena kwenye video za muziki.

Hamisa amesema kuwa ili aweze kutokea kwenye video ya wimbo wowote ule ni lazima uwe mzuri zaidi ya Salome ya Diamond ambao video yake ndio ya mwisho yeye kuonekana.

“Sifanyi video tu nimefanya, ninachagua. Ninachagua wimbo, nachagua maudhui, nachagua kila kitu, so for me kutokea kwenye video nyingine inabidi iwe nzuri zaidi ya Salome,” amesema Hamisa.

Video ya Salome kutokwa kwa Diamond Platnumz akishirikiana na Rayvanny ilitoka September 18, 2016 na hadi sasa ina views Milioni 23 katika mtandao wa YouTube.

No comments:

Post a comment