Saturday, 26 May 2018

Ronaldinho Kufunga Ndoa na Wachumba Wake Wawili Mwaka Huu

Gwiji wa soka nchini Brazil, Ronaldinho anatarajia kufunga ndoa katikati ya mwaka huu mwezi Agosti na kufanya sherehe moja na wachumba zake wawili, Priscilla Coelho na Beatriz Souza.

Watatu ambao wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani na furaha  kwenye jumba la kifahari la nyota huyo wa soka jijini Rio de Janeiro tangu Disemba mwaka jana.

Gazeti la O Dia la Brazil limeripoti kuwa Ronaldinho alianza mapenzi na Coelho miaka michache iliyopita kabla ya kumuona Souza mwaka 2016.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa wachumba zake hao wanapokea posho ya dola 2000 za kimarekani sawa na Shilingi Milioni 4.5 na zaidi kwa pesa ya kitanzania kutoka kwa Ronaldinho na amekuwa akiwapa zawadi zinazolingana yakiwamo manukato yanayofanana.

Ronaldinho hajawahi kuthibitisha uhusiano wake na wapenzi hao wawili lakini husafiri nao karibu katika matukio yote anayoalikwa limesema gazeti la  O Dia.

Aidha ndoa za wanawake wengi haziruhusiwi kisheria nchini Brazil, hivyo haijajulikana kwa gwiji huyo wa soka kama atafanikisha swala hilo la kufunga ndoa na wanawake hao ambao wameonesha kukubaliana na uamuzi huo

No comments:

Post a Comment