Tuesday, 29 May 2018

Rayvanny aeleza sababu za kumpa shavu Rosa Ree


Msanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Rayvanny ameeleza ni kwanii Rosa Ree ndiye rapper pekee wa kike katika remix ya ngoma yake ‘Pochi Nene’

Muimbaji huyo amesema kuwa kwanza amekuwa akivutiwa na muziki wa Rosa Ree, pili wimbo wenyewe ulimuhitaji Rosa Ree kutoka na aina yake ya rap.

“Nawakubali wasichana wote wanaorap lakini Rosa Ree is my favorite wangu naweza kusema lakini niliona kama atafaa zaidi kutokana na concept ya wimbo wenyewe,” amesema.


“Ukimsikia anavyo-sound kama Nicki Minaj sio Nicki Minaj, nikaona kwenye biti kama lile ataleta vibe na ndio maana nikaamua kumuweka,” Rayvannuy ameiambia Wasafi TV.

Poch Nene Remix imewakutanisha wasanii kama Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo Bizness, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.

No comments:

Post a comment