Tuesday, 15 May 2018

Rais Magufuli kuwakabidhi Simba kombe la VPL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, huwenda akawa mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 2018.

Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia, wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli akabidhiwe Kombe la Ubingwa wa Cecafa kwa Vijana Mei 19 Uwanja wa Taifa,Maombi ambayo yamepitishiwa kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Dkt.Harrison Mwakyembe.
Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.
Sherehe za ubingwa wa Simba na Serengeti Boys zinatarajiwa kuanza majira ya saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.

No comments:

Post a comment