Spika wa bunge wa zamani Pius Msekwa amesema kuwa kazi ya upinzani ni kukosoa na kuisaidia serikali katika kufikia maendeleo kama Katiba inavyoelekeza.

Msekwa ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha East Africa BreakFast kinachoruhwa na East Africa Radio kuwa utaratibu wa uendeshaji wa bunge la vyama vingi umeainishwa kwenye kanuni za Bunge.

“Wakati tunahama kutoka bunge la chama kimoja na kwenda bunge la vyama vingi tuliandaa kanuni mpya kwa lengo la kuhakikisha upinzani utakapokuwa bungeni utekeleze jukumu lake kikatiba ambalo ni kuikosoa serikali” amesema Msekwa

Msekwa ameongeza kuwa jukumu la upinzani haliishii kukosoa tu bali kuleta mawazo mbadala pia ili kuisaidia serikali kuu katika kutimiza wajibu wake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: