Monday, 21 May 2018

NGORONGORO HEROES YAPIGWA 4-1 NA MALI KABWILI AKIWA LANGONI, YATUPWA NJE KUELEKEA AFCON


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kimekubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Mali katika mchezo wa marudiano wa kufuzu kuelekea AFCON (U20) uliopigwa kwenye Uwanja wa Omnisports Modibo Keita mjini Bamako.

Matokeo hayo yanaifanya Ngorongoro kutupwa nje ya kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza AFCON mwakani huko Niger kufuatia kuruhusu idadi ya mabao 6-2 jumla.

Katika mchezo wa awali uliopigwa jijini Dar es Salaam Mei 13 2018, Ngorongoro walikubali kichapo cha mabao 2-0 huku mlinda mlango Ramadhani Kabwili akiwa nje.

Vilevile atika mchezo wa kwanza Kabwili hakuweza kucheza baada ya kutopangwa na Kocha Mkuu Ammy Ninje lakini alianza katika kikosi cha leo.

No comments:

Post a comment