Friday, 18 May 2018

Manara ajitolea kulipia viingilio kwa wasio na fedha hapo kesho, awaomba Yanga kujitokeza

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa yupo tayari kujitolea kiingilio kwa baadhi ya mashabiki watakao shindwa kufanya hivyo ili kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi.
Kupitia mahojiano yake na Radio EFM kipindi cha Sports HQ kinachoruka asubuhi, Manara ameeleza kuwa kwa wale baadhi watakaokuwa hawana fedha za kiingilio, atakuwepo getini na bunda le fedha kuwapatia Tshs 2000 kwa kila mmoja.
Licha ya kuwalipia kiingilio msemaji huyo mwenye mbwembwe zaidi kwenye klabu za soka hapa nchini, Manara amewaomba watani zake wa jadi Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanjani hata kama watakuja kuzomea nakusema kuwa hiyo ndiyo burudani ya soka.
Kwenye mchezo huo wa hapo kesho wa Simba dhidi ya Kagera Sugar ambapo watakabiziwa taji mabingwa hao wapya wa ligi kuu Tanzania Bara itahudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a comment