Wednesday, 16 May 2018

Lulu Aanza Kufanya Kazi za Jamii Jijini Dar


Msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.
 
BAADA ya kifungo chake jela kubadilishwa na kuwa kifungo cha nje, msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekuwa akifanya kazi ya usafi katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani jijijni Dar es Salaam tangu Jumatatu wiki hii.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mtandao huu, mrembo huyo amekuwa akifika makao makuu ya wizara hiyo asubuhi na kufanya majukumu yake na kuondoka mnamo saa 4 au 5, kabla ya mchana.

Baada ya kumaliza kazi zake hizo za kufagia na kudeki, Lulu ambaye hufika hapo kwa gari, pia huondoka kwa gari kurejea nyumbani.

Mwigizaji huyo alihukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba, lakini adhabu hiyo imebadilishwa na kuwa kifungo cha nje.

No comments:

Post a comment