Upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, umeomba Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kutupilia mbali mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa kuwa yanamapungufu, kisheria.

Maombi hayo yamewasilishwa leo Mei 16, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilabard Mashauri na Wakili Peter Kibatala, ambaye amewasilisha mapingamizi nane ya kisheria ‘yanayoshambulia’ uhalali wa hati ya mashtaka na mashtaka dhidi ya washtakiwa.

Katika Mapingamizi hayo, Kibatala amedai, kibali cha DPP kina mapungufu ya kisheria kwa sababu haioneshi imetolewa kwa mashtaka yapi na pia hati ya mashtaka imewataja majina washtakiwa wote bila ya kufafanua na pia imetaja tu kifungu cha sheria ambacho washtakiwa wameshtakiwa nacho huku akidai pia kwamba, hakuna kibali kilichowasilishwa mahakamani hapo kwa maana hiyo mashtaka dhidi ya washtakiwa yamepelekwa mahakamani hapo bila ridhaa ya DPP.
Aidha, Kibatala alitoa ombi mbadala na kuomba, iwapo mahakama itashindwa kuifuta hati nzima ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao basi iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria, likiwamo shtaka la nne, latano, la sita na la saba.

Alidai, maelezo ya mashtaka hayo yanawachanganya washtakiwa na hawawezi kujitetea ipasavyo, pia mashtaka hayo kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya (DPP) ambayo haipo kutokana na mapungufu hayo, inaonesha hakuna ridhaa yake.

“Kwa kuwa mashtaka hayo tajwa kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya DPP, lakini kuwa haipo tunaomba yafutiliwe mbali. Hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu shtaka la pili na la tatu hayana maelezo ya kutosheleza ya kuwapa washtakiwa msingi na uwezo wa kuweza kujitetea kikamilifu katika kesi hiyo ya jinai.

“Katika shtaka la kufanya mkusanyiko bila kibali hati haijataja watu waliotishiwa na kwamba wametajwa kwa wingi hivyo haijulikani ni washtakiwa ama ni watu wengine. Mashtaka yanayowakabili washtakiwa yamejichanganya na hayaonyeshi walipelekeaje kifo cha Akwilina na hao majeruhi walijeruhiwa na nani na kwa kutumia nini,” alisema Kibatala.
Amedai maelezo katika hati ya mashtaka yamerundikana kiasi kwamba ni vigumu mtu kujitetea na kwamba unapomshtaki mtu kwa kisababisha kifo ni lazima utoe Maelezo ya kutosha kuonesha unamaanisha kitu Fulani ili mtu aweze kujitetea.

Alidai mapungufu mengine yaliyomo kwenye hati hiyo ni kuwa hayaoneshi dhumuni la pamoja ambalo washtakiwa walikutana kulitenda hivyo linawanyang’anya washtakiwa haki ya kujitetea. Kibatala alidai kuwa hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu vifungu vilivyotajwa katika shtaka la Tatu, tano na saba siyo sahihi.

Alidai kuwa katika shtaka la kumi, kumi na moja na kumi na mbili yanamapungufu kisheria kwa sababu hayaonyeshi watu waliochochewa kufanya makosa ni wakina nani waliohudhuria mkutano, wakazi wa Kinondoni ama wapiga kura bila kujali itikadi zao.

Akijibu mapingamizi hayo, Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi aliiomba mahakama kuyatupilia mbali mapingamizi yote hayo ya upande kwa kuwa hayana mashiko kisheria.

Kuhusu kibali cha DPP kinachoipa mahakama ridhaa ya kusikiliza kesi, Kadushi alidai kuwa hakuna uamuzi wowote ulioweka msingi kwamba ni lazima kiwepo na nini ama hakipaswi kuwepo na nini.

katika kesi hiyo, mbali na Mbowe wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo Namba 112 ya 2018 ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicenti Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu
Upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, umeomba Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kutupilia mbali mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa kuwa yanamapungufu, kisheria.

Maombi hayo yamewasilishwa leo Mei 16, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilabard Mashauri na Wakili Peter Kibatala, ambaye amewasilisha mapingamizi nane ya kisheria ‘yanayoshambulia’ uhalali wa hati ya mashtaka na mashtaka dhidi ya washtakiwa.

Katika Mapingamizi hayo, Kibatala amedai, kibali cha DPP kina mapungufu ya kisheria kwa sababu haioneshi imetolewa kwa mashtaka yapi na pia hati ya mashtaka imewataja majina washtakiwa wote bila ya kufafanua na pia imetaja tu kifungu cha sheria ambacho washtakiwa wameshtakiwa nacho huku akidai pia kwamba, hakuna kibali kilichowasilishwa mahakamani hapo kwa maana hiyo mashtaka dhidi ya washtakiwa yamepelekwa mahakamani hapo bila ridhaa ya DPP.
Aidha, Kibatala alitoa ombi mbadala na kuomba, iwapo mahakama itashindwa kuifuta hati nzima ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao basi iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria, likiwamo shtaka la nne, latano, la sita na la saba.

Alidai, maelezo ya mashtaka hayo yanawachanganya washtakiwa na hawawezi kujitetea ipasavyo, pia mashtaka hayo kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya (DPP) ambayo haipo kutokana na mapungufu hayo, inaonesha hakuna ridhaa yake.

“Kwa kuwa mashtaka hayo tajwa kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya DPP, lakini kuwa haipo tunaomba yafutiliwe mbali. Hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu shtaka la pili na la tatu hayana maelezo ya kutosheleza ya kuwapa washtakiwa msingi na uwezo wa kuweza kujitetea kikamilifu katika kesi hiyo ya jinai.

“Katika shtaka la kufanya mkusanyiko bila kibali hati haijataja watu waliotishiwa na kwamba wametajwa kwa wingi hivyo haijulikani ni washtakiwa ama ni watu wengine. Mashtaka yanayowakabili washtakiwa yamejichanganya na hayaonyeshi walipelekeaje kifo cha Akwilina na hao majeruhi walijeruhiwa na nani na kwa kutumia nini,” alisema Kibatala.
Amedai maelezo katika hati ya mashtaka yamerundikana kiasi kwamba ni vigumu mtu kujitetea na kwamba  mtu kwa kisababisha kifo ni lazima utoe Maelezo ya kutosha kuonesha unamaanisha kitu Fulani ili mtu aweze kujitetea.

Alidai mapungufu mengine yaliyomo kwenye hati hiyo ni kuwa hayaoneshi dhumuni la pamoja ambalo washtakiwa walikutana kulitenda hivyo linawanyang’anya washtakiwa haki ya kujitetea. Kibatala alidai kuwa hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu vifungu vilivyotajwa katika shtaka la Tatu, tano na saba siyo sahihi.

Alidai kuwa katika shtaka la kumi, kumi na moja na kumi na mbili yanamapungufu kisheria kwa sababu hayaonyeshi watu waliochochewa kufanya makosa ni wakina nani waliohudhuria mkutano, wakazi wa Kinondoni ama wapiga kura bila kujali itikadi zao.

Akijibu mapingamizi hayo, Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi aliiomba mahakama kuyatupilia mbali mapingamizi yote hayo ya upande kwa kuwa hayana mashiko kisheria.

Kuhusu kibali cha DPP kinachoipa mahakama ridhaa ya kusikiliza kesi, Kadushi alidai kuwa hakuna uamuzi wowote ulioweka msingi kwamba ni lazima kiwepo na nini ama hakipaswi kuwepo na nini.

katika kesi hiyo, mbali na Mbowe wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo Namba 112 ya 2018 ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicenti Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini, Esterher Matiko, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Kesi bado inaendelea jioni hii, tutawahjuza kitakachojili. na Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini, Esterher Matiko, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Kesi bado inaendelea jioni hii, tutawahjuza kitakachojili.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: