Tuesday, 29 May 2018

KAULI YA SIMBA BAADA YA KUMNASA SALAMBA,


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Haji Manara, umesema usajili wa Adam Salamba ilioufanya ni trela tu, picha kamili linakuja.

Tayari Simba imeingia mkataba wa miaka miwili uliogharimu kiasi cha pesa, shilingi milioni 40 za kitanzania akitokea Lipuli FC ya Iringa.

Manara amesema usajili huo ni mwanzo tu wa silaha zake inazotarajia kuzileta baadaye huku akiahidi kuwa watashusha kifaa kingine kabla ya michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 3 2018 nchini Kenya.

Aidha, Manara ameeleza kuwa watasajili mchezaji mwingine hatari ambaye watakuwa naye kwenye michuano hiyo ya SportPesa huko Nairobi, Kenya.

Mbali na Kaheza, Simba tayari ilishanyaka saini ya Mshambuliaji wake wa zamani, Marcel Kaheza ambaye alikuwa akiichezea Majimaji FC.

No comments:

Post a comment