Tuesday, 29 May 2018

KAULI YA KIBABE KUTOKA KWA KLOPP JUU YA RAMOS KUMUUMIZA SALAH


Nyota wa Liverpool na Timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah amesema ana uhakika wa kuwepo kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kupata majeraha ya bega kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Real Madrid alipoumizwa na beki, Sergio Ramos.

Hata hivyo Ramos aliomba msamaha kwa Salah na mashabiki wote wa Liverpool kwa tukio hilo huku akimuombea apone haraka.

Licha ya Ramos kuomba radhi kwa Salah, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kitendo alichokifanya Ramos si cha kiungwana kwani inaonyesha alidhamiria kumuumiza Salah kwa kumwangusha kama anacheza mieleka.

Usiku wa Fainali, Salah, 25, aliondoka Uwanjani mjini Kiev akiwa analia baada ya kuchezewa rafu hiyo mbaya na Ramos. 

Liverpool walifungwa bao 1-3 na kuifanya Madrid kuchukua ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo.

”Upendo wenu na kuniunga mkono kwa pamoja vitanipa nguvu ninayoihitaji,” alisema Salah. Misri itacheza mchezo wake wa kwanza Juni 15 dhidi ya Uruguay katika Mji wa Yekaterinburg.

No comments:

Post a comment