Tuesday, 29 May 2018

Dk. Bashiru Ally achukua nafasi ya Kinana CCM

Hatimaye kile kitendawili kilichokuwa kikisubiriwa kupata majibu ya nani atarithi kiti cha aliyekuwa Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amepatikana Dk. Bashiru Ally ambaye ni Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa itikadi na uenezi (CCM) Humphrey Polepole imesema kuwa Dk. Bashiru ameteuliwa kwenye kikao cha Halmshauri Kuu ya chama hicho ambacho leo ni siku ya pili kinaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais Dk. John Magufuli.

“Chama cha Mapinduzi kinapenda kuuhabarisha umma kuwa kupitia kikao chake ambacho kimekaa siku ya pili leo kimemteua Dk. Bashiru Ally kuwa katibu mkuu wa chama na ndugu Raymond Mangwala kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)”, imesema taarifa

Aidha Polepole amesema kuwa Rais amependezwa na kazi iliyofanywa na Tume iliyoongozwa na Dk. Bashiru ya uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi.

No comments:

Post a comment