Friday, 11 May 2018

Alichojibu Barakah kuhusu harusi ya Alikiba, ‘Sijawahi kufikiria kuongea’

Muimbaji Barakah The Prince amefunguka sababu za kutohudhuria harusi ya Alikiba au hata kutoa pongezi kwa hatua aliyopiga msanii mwenzake ambaye walifanya wote kazi chini ya RockStar4000.

Kupitia Refresh ya Wasafi TV Barakah The Prince amesema hawezi kuongelea kitu hicho kwani hajafikiri kufanya hivyo.
“Siwezi kuongea chochote kwa sababu sijawahi kufikiria kuongea chochote, kwa hiyo sina comment,” amesema.
Katika hatua nyingine amesema hana mpango wa kufuatilia ngoma zake zilizobaki katika lable ya RockStar4000.
“Ni vitu ambavyo vimetokea na vimepita, kwa hiyo nadhani ambacho hakipo ni hakipo tu, hata kama nikizizungumzia siwezi kuzipata, hivyo sasa nashugulika na project zaungu binafsi,” amesema Barakah The Prince.
July 21, 2017 Baraka The Prince alijitoa kwenye chini ya usimamizi wa RockStar4000 kwa kile alichoeleza kuwa kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa katika label hiyo

No comments:

Post a Comment