Wanawake wanaosubiri kujifungua (wajawazito) na waliojifungua katika kituo cha afya cha ngarenaro halmashauri ya jiji la Arusha Mkoani Arusha wanalazimika kulala wawili katika kitanda kimoja kutokana na upungufu wa vitanda.


Wakizugumza na vyombo vya habari baada ya kutembelewa na naibu waziri wa Elimu William Olenasha wameiomba serikali kuwasaidia tatizo hilo ambalo limekuwa changamoto kubwa kituoni Hapo.

Wamesema kuwa wanalala wakiwa na watoto wao na nyakati za usiku kuna wakati huangukia chini kutokana na kujigeuza kutokana na vitanda kuwa vidogo na visivyoweza kuhimili watu wa wili kuvilalia.


“Hapa usiku tunanguka chini kwasababu tukipata uchungu mtu anageuka geuka lakini sasa unaanguka chini na unaona vitanda vya Hospitali ni Vidogo sana tunaomba waziri afikishe jambo hili serikalini”alisema mmoja wa kinamama hao waliokuwa katika wodi hiyo.

Wamesema kuwa kwenye kituo hicho huduma ni nzuri inayotolewa na madaktari na manesi lakini tatizo la kulala wawili ndiyo limekuwa kero kubwa.

Naye Afisa muuguzi mkuu wa kituo hicho Dk.Hosea Naamani alipozungumza na Naibu waziri Mh.Ole Nasha alisema kuwa wana changamoto ya ufinyu wa Wodi ya wazazi lakini pia Uchache wa Vitanda katika Wodi iliyopo,Lakini changamoto hizo haziwazui waokutoa Huduma nzuri ya Afya kwa wakina Mama wote wanaofika kupata Huduma ya Kujifungua katika Kituo chao Cha Afya.

Baada ya kuzisikia changamoto Mh.naibu waziri aliwapapongeza wahudumu wote kwa kazi wanazoendelea kuzifanya na kuwahidi kuwa changamoto zote ataendelea zifikisha sehemu husika ili zifanyiwe kazi kwa wakati.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: