Na Filbert Rweyemamu

Nchi za Tanzania na Uganda licha ya kuwa ndizo zinazozalisha nusu ya zao la ndizi  barani Afrika zenye thamani ya dola 4.3 bilioni (sawa na Sh  9.4 Trilioni) kwa mwaka bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo magonjwa ya migomba na soko la uhakika.


Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa wataalamu wa utafiti wa migomba kwenye nchi za Maziwa Makuu jijini Arusha ,Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela(NM-AIST),Profesa Kalori Njau alisema jitihada za dhati zimekua zikichukuliwa kukabiliana na magonjwa ya migomba ukiwemo mnyauko fuzari.


Katika mkutano huo ulioandaliwa na taasisi ya kimataifa ya Mazao ya Tropiki(IITA) umewaleta pamoja wataalamu kutoka mataifa mbalimbali wanaotekeleza mradi  wenye lengo la kuongeza uzalishaji wa ndizi katika nchi za Tanzania na Uganda.


Profesa Njau alisema ili kuwawezesha wakulima wadogo kuongeza uzalishaji wadau mbalimbali hawana budi kutoa elimu ya matumizi sahihi ya miche bora iliyofanyiwa utafiti ambayo ina ukinzani dhidi ya magonjwa yanayoshambulia migomba.


"Ndizi ni zao muhimu sana hapa nchini kutokana na kuwa na wazalishaji katika mikoa sita ambayo ni Kagera,Kilimanjaro,Arusha,Mbeya,Tanga na Morogoro na linalimwa kwaajili ya chakula lakini pia kwaajili ya biashara,"alisema Profesa Njau


Alisema wataalamu hao wanajadili namna ya kuliongezea tija zao hilo ili kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji kutoka asilimia tisa ya sasa hivi hadi 30 ili litoe mchango muhimu katika uchumi wa wakulima wadogo katika nchi za Maziwa Makuu.




Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: