Tuesday, 24 April 2018

Vanessa Mdee atoa neno baada ya ‘Wet’ kufikisha views 1M

Japo imekuwa siyo jambo geni tena kuona video ya Bongo Flava kufikisha views milioni moja YouTube lakini imekuwa siyo kazi rahisi kuweza kuifikia namba hiyo hasa katika kipindi kifupi zaidi.
Basi Vanessa Mdee amefikia namba hiyo kupitia video ya wimbo wake mpya ‘Wet’ ambao amemshirikisha G Nako tena ndani ya wiki mbili pekee.
Msanii huyo hakutaka jambo hilo liweze kumpita kiurahisi bila kutoa neno lolote. Vee Money kupitia mtandao wa Instagram amewashukuru mashabiki wake huku akiongeza kuwa kufikisha views hao kwake ni kitu kikubwa sana.

No comments:

Post a Comment