Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga katika Ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma.

Katika mazungumzo yao  Dkt. Kolimba amemwahidi Spika wa EALA kuwa, Wizara na Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa na lengo la kuboresha ushirikiano baina ya nchi wanachama wa EALA.

Kwa upande wake Spika wa EALA amesema kuwa, kwa sasa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na Mabunge ya Nchi wanachama na kutoa mrejesho kwa Nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya yanayojili katika Bunge hilo.

Spika Ngoga yupo Mkoani Dodoma ambapo Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mjini humo ambavyo vimeanza April 9 na vinatarajiwa kumalizika April 28
Share To:

msumbanews

Post A Comment: