Wednesday, 25 April 2018

Serengeti Boys kukipiga na Kenya Leo

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' leo Aprili 25, 2018 wanatarajia kutupa karata yake nyingine muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya nchini Burundi.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Afisa wa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari wa Jijini Dar es Salaam jana katika kuelekea mchezo huo.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni kwenye dimba la Muyinga nchini Burundi.

Serengeti Boys walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.

Kufuzu hatua ya nusu fainali Serengeti Boys walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.

No comments:

Post a comment