Tuesday, 10 April 2018

Nyumba 12 zasombwa na maji Mto Msimbazi

Nyumba 12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi,Mtaa Majengo Eneo la Vingunguti jijini dsm zimesombwa na Maji na huku nyingine zaidi ya 100 ziko hatarini kuanguka kutokana na Mmomonyoko wa Udongo unatokana na kupanuka kwa Mto Msimbazi na kuingia katika makazi ya watu.

Wakizungumza na Chanelten baadhi ya wananchi wanaoishi katika mtaa huo wamesema hali ni mbaya katika eneo hilo, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha huku mto huo ukiendelea kutanuka baada ya kuacha njia yake ya asili na kuingia katika makazi yao.

Diwani wa Eneo hilo Omar Kumbilamoto amesema walifanya juhudi za kupambana na mto huo kwa kuwashirikisha wananchi ambao kiasi cha Million 2 zilichangwa, lakini alidai baadhi ya watumishi katika manispaa hawakuonyesha ushirikiano na kuomba wizara ya mazingira chini ya ofisi ya makamu wa rais kuingilia kati.

No comments:

Post a comment