Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema kutua kwa ndege ya Emirates Airbus A380-800 kumewaongezea kujiamini katika biashara ya usafiri wa anga duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema leo Aprili 27, jijini Dar es salaam kuwa Emirates walichagua uwanja wa JNIA Dar es Salaam kutokana na kuzingatiwa kwa vigezo vya kimataifa vya uwanja huo.
 
Ndege hiyo  inalotajwa kuwa moja ya ndege kubwa duniani, ilitua kwa dharura JNIA Aprili 24 kutokana na hali mbaya ya hewa Mauritius, ilikokuwa ikielekea.

 Hata hivyo ndege hiyo iliondoka Aprili 25 kwenda Mauritius.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: