Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia baadhi ya wabunge wake, wameibua tuhuma nzito juu ya tabia chafu inayofanywa na wamiliki wa majumba yanayotumika kutibu waathirika wa madawa ya kulevya (sober house), kitendo kinachozidi kuwaathiri vijana wakiwa humo.

Akizungumza Bungeni kutaka maelezeo kutoka kwa serikali inachukua hatua gani juu ya hilo, Mbunge Kijana Halima Bulembo amesema kwamba wamili wa majumba hayo wana tabia ya kuwachoma tena sindano za madawa ya kulevya vijana ambao wanakaribia kupone ili wasitoke, na lengo kubwa likiwa ni kuendelea kuingiza pesa kupitria wao.

“Kumekuwa na malalamiko mengi ya waathirika wa madawa ya kulevya wanapokuwa rehab, wanapokaribia kupona wahusika wanawachoma dawa tena za madawa ya kulevya ili wasiweze kutoka lengo likiwa waendelee kijipatia fedha”, amesema Halima Bulembo.

Taarifa hiyo iligongewa msumari na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama, kwa kusema kwamba malalamiko hayo sio mara ya kwanza Bungeni, na kutoa onyo kali kwa wamiliki.

“Tumepokea hii taarifa sasa kwa mara kadhaa, waheshimiwa wabunge wametuarifu kwamba upo mchezo mchafu unaoendelea kwenye sober house, badala ya kuwasaidia vijana wetu wapone, na waondoke sober house, lakini wamiliki wanataka kuendelea kuwaweka pale kwa faida yao binafsi. Nitoe agizo kwa wamiliki wa sober house ambao wana mchezo huo kuacha haraka, na naagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na yeyote atakayebainika kufanya jambo hilo tutamchukulia hatua kali”, amesema Waziri Jenista Mhagama.

Kwa upande wa serikali wamesema hawajapokea taarifa hizo rasmi kwa sababu asilimia kubwa ya sober house zinamilikiwa na watu binafsi, lakini imeweka miongozo kusaidia soiber house, na kuhakikisha kuwa mpango wa serikali kuwa na sober house nyingi inazomiliki unafanikiwa ili kuondokana nalo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: