Monday, 9 April 2018

BREAKING NEWS: WATU 8 WAFARIKI AJALINI MBEYA


WATU nane wamefariki dunia papo hapo na mmoja amejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Toyota Noah kugongana na basi katika eneo la Igodima nje kidogo ya Jiji la Mbeya. Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya, Mussa Taibu amethibitisha.
Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Aprili 9, 2018 mchana ikihusisha Noah yenye namba za usajili T 649 DEA na basi la Igembesabo katika Barabara ya Chunya Mbeya huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijulikani.
Endelea kufuatilia habari zetu kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a comment