Monday, 5 March 2018

Watu watano wajeruhiwa kwenye shindano la magari Tanga


Watu watano wamejeruhiwa katika mashindano ya mbio za magari mkoani Tanga jana Jumapili asubuhi baada ya mmoja wa madereva wanaoshiriki mashindano hayo kushindwa kulimudu gari lake na kuparamia watu waliokuwa kando wakishuhudia mashindano hayo.

Baada ya tukio hilo kutokea baadi ya watu walimfuata dereva huyo aliyekuwa na presha kubwa ya kuhofia huenda amesababisha kifo kwa watazamaji hao ambapo walimsihi atulize presha.

No comments:

Post a comment