Thursday, 15 March 2018

Msanii Afande Sele Ajiunga na Ccm

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongofleva Selemani Msindi (Afande Sele) ametangaza rasmi kujiunga na chama cha mapinduzi CCM mbele ya Rais Magufuli siku ya leo March 15, 2018 wakati alipokuwa aki-perform mbele ya Rais na wananchi Morogoro rais alipokwenda kuzindua Kiwanda cha Sigara.
Afande Sele baada ya kutangaza hivyo amepokelewa rasmi na viongozi wa Chama hicho cha Mapinduzi mkoani Morogoro mbele ya Rais Magufuli, huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza mahali hapo, Afande Sele amemuahidi Rais Magufuli kuwa kuanzia leo atakuwa naye sambamba kuleta maendeleo taifa.

No comments:

Post a comment