Zikiwa zimebaki takribani siku tano kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni, Siha na Kata nane Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, imedai maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa pamoja na kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitoka

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima amesema hayo mara baada ya kikao na watendaji wa tume kabla ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika jumamosi ijayo (Februari 17).

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya elimu ya mpiga kura mfululizo hadi siku ya uchaguzi, elimu ambayo itakua ikigusia mada mbalimbali za uchaguzi ikiwemo haki na wajibu wa mpiga kura, wakala wa vyama vya siasa na msimamizi wa uchanguzi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: