Tuesday, 20 February 2018

SIMBA BAADA YA USHINDI WA LEO ,HII NDIYO TIMU ITAKAYOKUTANA NAYO HATUA INAYOFUATAMafarao wa Misri, Al Masry wameangukia pua baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Hata hivyo, Al Masry wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya ushindi wao wa mabao 4-0 wakiwa nyumbani Misri na sasa hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho, wanakutana na Simba.

Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendamarie na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa idadi ya mabao 5-0.

Maana yake, Simba inakwenda kukutana na mlima mwingine raundi ya mapema tu baada ya kurejea katika michuano ya kimataifa.

Mechi ya kwanza itaanzia jijini Dar es Salaam, kabla ya Simba kufunga safari na kwenda Misri kumalizia ngwe hiyo inayotarajia kuwa ngumu.

Simba ina heshima kubwa kwa kuwa imewahi kuivua ubingwa na kuing’oa mashindano Zamalek ya Misri, timu kubwa ya pili na moja ya klabu maarufu barani Afrika.

No comments:

Post a comment