Friday, 23 February 2018

Serikali yaagiza ukaguzi wa magari binafsi


Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza leo kwamba kuanzia tarehe 1 Machi 2018 kuwa utaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.
Akizungumza leo na wanahabari, Mh. Masauni amesema kwamba Wamiliki wa magari madogo wanatakiwa kupeleka magari yao katika vituo vya polisi ili yafanyiwe Ukaguzi kama yanastahuili kuendelea kuwepo barabarani.
Aidha Mh. Masauni amewaonya maaskari kuhusu zoezi hilo kwa kuwaambia kwamba "Askari yoyote atakayetumia nafasi yake kutoa stika ya gari bila kulifanyia ukaguzi na ilihali halina vigezo vya kupewa stika nataka niwaambie kuwa huu si wakati wake, zama zimebadilika".
Pamoja na hayo Mh. Masauni ameongeza kwamba "Nataka madereva  wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja".
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Fortunatus Musilimu amesema katika Ukaguzi wa magari madogo utakaoanza mwezi ujao, mtu atakaekiuka na kukataa kupeleka gari lake kufanyiwa ukaguzi atakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.

No comments:

Post a comment