Wednesday, 21 February 2018

Mkuu wa wilaya ampongeza mumewe kwa kuongeza mke


Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah, ameushangaza umma baada ya kumpongeza mume wake kwa kuongeza mke wa pili, kwani ni kitendo cha nadra sana kwa wanawake kufanya hivyo licha ya kuwa misingi ya dini inaruhusu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkuu wa wilaya huyo ameandika ujumbe huku akiujulisha umma kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.

“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu  kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi”, ameandika Bi. Zainab Abdallah.

Mheshimiwa huyo wa serikali ya wamu ya tano aliendelea kuandika kuwa ...”Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu      mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.
Alichokiandika DC Zainab kwenye ukurasa wake wa instagram

No comments:

Post a Comment