Tuesday, 27 February 2018

Mhe. Mbowe : Hukumu ya SUGU ilipangwa hotelini, Mkuu wa Mkoa Mbeya alihusika

Mhe. Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amedai kuwa hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘SUGU’ ilipangwa hotelini siku 4  kabla ya mahakama kutoa hukumu.
Mhe. Mbowe amesema kuwa suala hilo lilipangwa na hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala alilijua hilo kuwa SUGU atafungwa huku akimtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala kuhusika.
“Hukumu ya SUGU ilifahamika na ilipangwa hotelini, kwamba Sugu anafungwa miezi mitano tulipata taarifa hizo siku 4 kabla. Na kwamba polisi walikusanywa mkoa mzima wa Mbeya, Mkoa mzima wa Songwe, watu wa usalama wa taifa wakajazwa Mbeya kukabiliana na presha ya wananchi ni jambo liliratibiwa. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anauhusika na anajua jambo hili, Amosi Makala,”amesema Mhe. Mbowe leo Jumanne kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za makao makuu Jijini Dar es salaam .
Soma zaidi kuhusu hukumu – SUGU apigwa miezi mitano jela 
Kwa upande mwingine Mhe. Mbowe amesema kuwa CHADEMA hawaingilii maamuzi ya mahakama bali wanawasema baadhi ya watendaji wa mahakama wanaotumika kisiasa.
Tunaiheshimu sana mahakama, Muhimili wa mahakama ndio muhimili ambao unasaidia wa Kuregulate nchi, lakini mahakimu mmoja mmoja wanapotumika ndio wanaichafua mahakama na wanalichafua taifa,“amesema Mbowe.

No comments:

Post a comment