Kikundi hicho kilikusudia kuwafikisha mahakamani wasanii hao lakini kabla ya kuchukua hatua hiyo Aslay na Nandy wakiwakilishwa na kiongozi wao walifika visiwani humo na kufanya mazungumzo na kikundi hicho ambapo wamehitaji kulipwa milioni tano. 
Katibu Mkuu wa kikundi cha utamaduni cha tarabu asilia, Taimur Rukuni Twaha, amesema kikundi  hicho cha tarab kimewataka wasanii hao kulipa faini kutokana na kuimba wimbo huo bila ya ridhaa yao, pia amedai kuwa wamekubaliana leo Alhamisi na kufikia muafaka huo baada ya wasanii hao kupitia kwa kiongozi wao kukiri kufanya kosa hilo. 
Twaha amesema licha ya kukiri makosa hayo pia meneja huyo wa Aslay ameomba kuingia mkataba na kikundi hicho cha tarab kufanya biashara ya kuziimba tena nyimbo zao zengine za zamani.
Katibu huyo amesema kuhusu nyimbo zao kuimbwa tena hilo bado hawajaafikiana kwa sababu walishapewa agizo na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dk Salmin Amour Juma wakati akiwa rais, kuwa wasikubali nyimbo zao za tarabu asilia kuzibadili na kuzifanya katika mfumo wa muziki wa kisasa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: