Teddy kilanga

Serikali imetenga kiasi cha sh.13.3 Trilioni sawa na asilimia 37 ya  bajeti ya Taifa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2020/2021 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya miundombinu nchini.Akizungumza wakati akifungua kongamano la 31  la kitaifa la Taasisi ya wahandisi Tanzania (IET) uliofanyika wilayani Arumeru mkoani Arusha Waziri wa ujenzi  na uchukuzi ,Profesa Makame Mbarawa alisema


kuwa serikali imejipanga kuwekeza zaidi katika sekta hiyo katika kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati."Serikali katika utekelezaji wake  itakuwa bega kwa bega katika kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wahandisi nchini


kwani kumekuwepo na utekelezaji wa miradi  unaofanywa na wahandisi hao katika maeneo mbalimbali na hiyo ni kutokana na sekta hiyo kuwa ya muhimu na nafasi kubwa ,"alisema
Aidha aliwataka wahandisi  kuwa wabunifu na kuongeza weledi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kitaifa kwani sekta hiyo inayonafasi  kubwa katika ukuaji wa kitaifa katika kuendelea kuwekeza katika ikiwa wahandisi ndio uti wa mgongo wa nchi yetu kwa ujumla.

Hata hivyo alisisitiza kuwa na utayari katika kazi zao ili waweze kuwa na ushindani mzuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali wanayoitekeleza na kuweza kuleta  tija kwa Taifa.Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa, Taasisi hiyo ni  muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu kwani imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikileta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.Kwa upande wake Rais wa  Taasisi ya wahandisi Tanzania  ,Injinia Sayed Qadri alisema kuwa, Taasisi hiyo ilianzishwa kwa madhumuni ya kukuza fani ya uhandisi ,sayansi na teknolojia nchini huku malengo hayo yakitekelezwa na wanachama wote kwa kupitia vitengo mbalimbali vikiwemo kitengo cha wahandisi wanawake,kitengo cha wahandisi wanajeshi,kitengo cha wanafunzi na kitengo cha mafundi .Alisema kuwa,mpaka sasa Taasisi ina jumla ya wanachama hai 4,568 ambapo idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na jumla ya wahandisi waliosajiliwa na Bodi ya usajili wa wahandisi kwani mpaka sasa jumla ya wahandisi waliosajiliwa na Bodi ni 32,145 ."Tunatoa wito kwa wahandisi na mafundi wote ambao bado hawajajiunga na Taasisi wajiunge ,kwani mpaka sasa ina jumla ya 279 tu wanachama ambao ni wahandisi wanawake,huku akiwataka wanawake kujiunga na Taasisi kwani wingi wa wanachama ndio mafanikio ya Taasisi."alisema Rais.

Share To:

Post A Comment: