Monday, 8 November 2021

RC SOPHIA MJEMA AONYA WANAOPANDISHA BEI YA VIFAA VYA UJENZI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Sophia Mjema ametoa onyo kwa wafanyabiashara ambao wameanza kupandisha bei za vifaa vya ujenzi ikiwemo Saruji, Nondo na Mabati na kusababisha zoezi la ujenzi miradi ya fedha za UVIKO-19 zilizotolewa na Serikali kuanza kupata changamoto.


Mjema ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa mabweni na madarasa mawili katika shule ya sekondari Kishapu ambapo ameeleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kupandisha bei za vifaa vya ujenzi kinyume cha utaraibu na kumuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza kuwashughukikia wote wanaokiuka bei halali ya bidhaa hizo kwa makusudi.

No comments:

Post a Comment